Music

Audio Music: Jessica Bm – Furaha Yangu

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu leo kutoka jiji kubwa la Dar es salaam, nimekusogezea wimbo uitwao ”Furaha Yangu” kutoka kwa moja ya mwimbaji mahiri na anayefanya vyema sana katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania na huyu si mwingine bali ni Jessica Bm Honore, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Still Alive zilizopo jijini Nairobi nchini Kenya.

Kupitia channel ya Youtube mwimbaji Jessica Bm aliandika:-

”Furaha yangu ni wimbo washukrani kwa Mungu, kuna maisha Mungu amekupatia si kwa sababu ya chochote ulichofanya cha thamani kwa Mungu, ila ni Neema na upendo wake, binafsi nimegundua Mungu wangu ndio Furaha ya kweli, na sioni haya kumpa sifa hiyo, ungana nami kumfurahia Mungu katika maisha yetu. wimbo huu ume rekodiwa nchini kenya, studio za still alive records, wimbo umeandikwa na mimi Jessica honore. barikiwa…share comment, SUBSCRIBE, like. God bless you.” – Alimaliza Jessica Honore Bm

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao kwa hakika utakupa nafasi nyingine ya kumtukuza Mungu kwa kiwango cha tofauti na cha kipekee sana. Karibu ubarikiwe!!

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Jessica Bm kupitia
Simu/WhatsApp: +255 712 332 007
Facebook: Jessica Honore bm
Instagram: @officialjessicah
Twitter: jessicabm
YouTube: Jessica Honore bm

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Audio Music: Ivan Mosha - Siku Hazigandi

Next post

Audio Music: Tim Godfrey - Walking Miracle