Music

Audio Music: The Gratitude – RABABA-EH

Kutoka kwa kundi la waimbaji wa Muziki wa Injili kwa mtindo wa kisasa mjini Lagosa nigeria wakifahamika kwa jina la The Gratitude, kwa mara ya kwanza wameachia wimbo wao wa kwanza uitwao RABABABA-EH.

Huu ni wimbo unaotarajiwa kuwa kwenye albamu yao mpya wanayotajarajia kuiachia hivi karibuni, ukiwa ni wimbo pekee unaohimiza watu kusali ukiwa na mchanganyiko wa aina za muziki wa rap, trap na soul.

Kundi la The Gratitude liliundwa mwaka 2016 chini ya uongozi wa kanisa la  The Commonwealth of Zion Assembly lililopo mjini Lagos Nigeria, ambapo kulifanyika mchakato wa uteuzi uliofanywa na Tye Tribbett(mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini marekani) na Tim Godfrey(Music Director kutoka nchini Nigeria) na kufanikiwa kupata waimbaji 16 ambao ndio wanaunda kundi hili la The Gratitude.

Tangu wakati huo, wameandika nyimbo nyingi zilizofanya vizur sana na kuwawapa mafanikio makubwa kupitia matamasha ambayo wamefanya duniani kote, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, Dubai na Uingereza.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakwenda kukubariki. Karibu!!

 

Download Audio

Social Media
Facebook: The Gratitude COZA
Instagram: @thegratitudecoza
Twittter: @thegratitudecoza

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Je unafahamu umuhimu wa kuwa na taarifa? - Mwal.Tuntufye A. Mwakyembe

Next post

Audio Music: Shalom Obosa – My Case is Different