Habari

Aniset Butati Aweka Historia ya Uzinduzi wa Albamu yake Jijini Dar.

Staa  wa muziki wa Injili Tanzania, Aniset Butati ameweka historia ya kufanya uzinduzi wa Albamu yake inayofahamika kwa jina la ” WATAULIZANA’‘ yenye jumla ya nyimbo nane.

Akizungumza na Gospo Media mara baada ya kumaliza uzinduzi wake alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kufanikisha lengo lake la kufanya uzinduzi jambo ambalo amekuwa akiliombea siku zote.

Uzinduzi huu ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwani si kwa akiri zangu bali yeye pekee Mungu ndio wa kushukuriwa sana maana unaweza ukapanga hivi yeye akapanga vile sasa inapotokea umefanikisha kama hivi una mshukuru Mungu sana, pia jambo jingine la kuwaambia wadau wa muziki wangu uzinduzi ulikuwa na lengo kubwa la kuchangisha pesa ili niweze kufanikisha Albamu yangu hii ikiwa ni pamoja na kumalizia kufanya video ya baadhi nyimbo ambazo bado sijazifanikisha “Alisema Aniseti Butati.

Butati alifanya uzinduzi wake katika kanisa la T.A.G Mwenge siku ya tarehe 23 mwaka huu na kuhudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo waimbaji mashuhuri wa hapa nyumbani kama vile Joshua Makondeko, Jessica Honore, Kasaki Kingwangwa, Giveness Ngao  na wengine wengi.

Kwa mawasiliano na Aniset Butati:

Simu/WhatsApp: +255 675 197 388
Facebook: Aniset Butati
Instagram: @anisetbutati
YouTube: Aniset Butati

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram > @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Audio: Phoebe Carol - Baraka Zako

Next post

Download Audio: Sampamba - Thamani